Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaboresha bei ya ardhi inayotwaliwa na Migodi ili iendane na thamani ya ardhi ya eneo husika?
Supplementary Question 1
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nina maswali mawili ya nyongeza. Wananchi wa maeneo yote ambayo yanazunguka mgodi wa Barrick North Mara hawajui kwamba ardhi ndiyo ya kwao kilichopo chini siyo cha kwao.
Je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kwenda kufanya mkutano katika eneo lile ili kutoa elimu hii kwa wananchi ili wajue kwamba hawahusiki na dhahabu iliyoko chini ya ardhi ile?(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, pamoja na manung’uniko makubwa sana ya eneo hilo ni nili wananchi wa eneo la Nyamichele, Murwambe, Nyabichune na Kiwanja watalipwa fidia yao? Ahsante.
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Waitara, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwenda kwenye eneo, yaani uwandani Wizara tuko tayari kwenda na tutawasiliana nae kwa ajili ya kupanga utaratibu wa jinsi ya kufika kule kwake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu fidia ya maeneo aliyoyataja nitawasiliana nae kujua viwango vya hatua zilizofikiwa hadi sasa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved