Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Simon Songe Lusengekile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busega

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. NJALU D. SILANGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Mahakama ya Ardhi chini ya Muhimili wa Mahakama?

Supplementary Question 1

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ahsante kwa majibu ya Serikali.

Kwa kuwa, ufanisi wa Mabaraza umekuwa mdogo sana kwa sababu hayapo kila Wilaya, ukilinganisha kwa mfano Itilima wanapata huduma Maswa, Meatu wanapata huduma Maswa na tumefanya wanachi kuingia gharama kubwa bila sababu za msingi. Ukisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Ibara ya 74(1) ukurasa wa 179, imeeleza kwamba Mabaraza haya sasa yahamishiwe kwenye Muhimili wa Mahakama.

Je, ni lini Serikali itaanza mchakato huo na kuukamilisha mapema?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ninakushukuru na naomba nijbu swali moja la Mheshimiwa Simon Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Simon kwa kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Wizara yetu ya Katiba na Sheria pamoja na Wizara ya Ardhi pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama na mfumo mzima wa Mahakama wako kwenye hatua za mwisho za kukamilisha mjadala huu wa kuhamishia Mabaraza haya kwenye Muhimili wa Mahakama kama ambavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeeleza. Ahsante.