Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, Serikali imejipanga vipi kushughulikia malalamiko kuhusu kikototoo?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kikokotoo, issue siyo elimu, issue ni ile percent inayotolewa. Watu wanalalamikia percent inayotolewa kwamba hawajakubaliana nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; tuna malalamiko kutoka kwa kundi muhimu la wafanyakazi ambao wote tunajua historia ya wafanyakazi ndiyo hasa kundi kubwa lililokuwa likifanya mapinduzi mbalimbali, sehemu mbalimbali duniani. Sasa ni lini Serikali pamoja na majibu iliyoyatoa, itafanya ile ujumuishi? Kwa sababu wafanyakazi waliostaafu pia wanasumbuka sana. Wapo ambao walikuwa NSSF wakahamishiwa PSSSF, wanapokwenda kudai mafao yao wanalipwa kidogo na PSSSF na wanatakiwa tena kuanza kufuatilia NSSF; imeleta usumbufu mkubwa. Ninyi kama Serikali mmejipangaje kuwasaidia ili walipwe kwa pamoja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Askari wetu au Jeshi la Polisi, wao ni kama majeshi, lakini kikokotoo hiki kinaoneka kwamba hakiwahusu majeshi mengine, isipokuwa askari wameingizwa kwenye kikokotoo hiki, nao hawakubaliani na hiyo. Wanasema kwa nini wao wasiwe regarded kama majeshi mengine yalivyokuwa regarded? Ahsante.

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Msambatavangu alivyoeleza, ni kwa sababu tu ya pengine taarifa kuwafikia watu vizuri na ndiyo maana wakati wote kumekuwa na mkakati wa kutoa elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali watumishi waliokuwa wakichangia kwa asilimia 25, kama alikuwa anapata shilingi milioni 46, kwa sasa malipo ya mkupuo analipwa shilingi milioniā€¦; wakati huo alikuwa analipwa shilingi milioni 44 na katika pensheni ya kila mwezi alikuwa analipwa shilingi 800,000. Kwa mabadiliko haya ya sasa ambayo yalikubaliwa na wadau wote pia wakiwemo vyama vya wafanyakazi, katika asilimia 33, ukiangalia mkupuo umeongezeka. Ukiangalia mchango wake ule wa milioni 46 sasa hivi analipwa milioni 58. Pia ongezeko lingine kwenye pensheni ya kila mwezi, analipwa zaidi ya shilingi 700,000. Kwa hiyo, unaweza ukaona utofauti ambao umekuwepo hapo katika hiyo. Umekuwa na faida. Zaidi ya asilimia 81 kwa sasa wananufaika na mpango huu. Lilifanywa hili baada ya kushirikisha wadau, kwa sababu asilimia 31 ndio wamekuwa wanufaika wa kikokotoo hiki kipya. Kumbuka tulikuwa asilimia 25, tumekuja asilimia 33.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna faida nyingine ya kutengeneza uendelevu wa mifuko. Hii mifuko utakumbuka, awali kulikuwa kuna mifuko mingi; LAPF, tulikuwa tuna PSSF, na mifuko mingine mingi. Wajibu wa Serikali na agizo lililotolewa ilikuwa ni kuangalia ile faida kwamba hii mifuko itakuwa inaendeshwa lakini mwisho wa siku wanachama wake wapya hawawezi kunufaika nayo kwa sababu ya kutokuwa na ustahimilivu au stability ya mifuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kilichofanyika ni kuunganisha mifuko ili kutengeneza utaratibu ambao utawasaidia zaidi wanachama kuweza kunufaika na ndiyo maana tukawa na skimu hizo mbili. Moja ya upande wa wafanyakazi wa Serikali ambapo ni PSSSF na pili NSSF inashughulika na wale ambao ni watumishi katika kada za kawaida. Kwa hiyo, faida ni nyingi kuliko hasara kwa kipindi hiki. Walioongezeka hapo ni asilimia 81 ambao wanapata faida zaidi hasa kwenye mkupuo ule wa mwisho, imekuwa fedha wanayolipwa kwenye mkupuo ni kubwa zaidi, ahsante.