Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: - Je, lini Serikali itakarabati miundombinu chakavu ya maji na kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kutosha katika Mji wa Mbinga?
Supplementary Question 1
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafsi ya kuuliza swali la nyongeza. Lakini pia nichukue nafasi hii kuishukuru sana Serikali kwa utekelezaji wa hiyo miradi. Pia nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi zake nzuri. Alifika Mbinga, na wakati huo amekuja kukagua vyanzo vya maji aliona hali halisi ya mahitaji ya maji katika Mji wa Mbinga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja la nyongeza. Pamoja na Serikali kusema kwamba imeanza kufanya ukarabati kilometa 21 na kununua dira za maji 2,500 kiwango hiki bado ni kidogo. Nilitaka nijue, sasa Serikali ina mpango gani wa kuongeza fedha ili kuhakikisha kwamba ukarabati ule unaendelea katika Mji wa Mbinga? Ahsante.
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Mbinga kwa kazi kubwa na namna ambavyo anawapigania wananchi wake. Nataka nimhakikishie na ukisoma maandiko ya dini kwa maana ya Mathayo 7:7 yanasema: “Ombeni nanyi mtapewa, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa.”
Nataka nimhakikishie tutaiangalia Mbinga kwa namna ya pekee ili kuhakikisha wananchi wake wanapata maji. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved