Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Shukuru Jumanne Kawambwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bagamoyo
Primary Question
MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA aliuliza:- Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa mipaka kati ya TANAPA na vijiji na vitongoji jirani vinavyowazunguka.Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza mgogoro huu kati ya TANAPA na vitongoji vya Kitame, Razaba, Gama-Makani katika Kata ya Makurunge?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. SHUKURU KAWAMBWA: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu ingawa ni majibu ambayo mimi na wananchi wangu wa Bagamoyo yanatupa matatizo. Sasa naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kama atakubali kuielekeza timu hii ya pamoja iliyoundwa ili iweze kukutana na wawakilishi wa wananchi hawa akiwemo Mbunge na Waheshimiwa Madiwani wa jimbo la Bagamoyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, TANAPA inawatoza fedha wananchi wa Makurunge na Matipwili wanapovuka daraja eneo la Gama katika Mto wa Wami wanapokuwa wanafanya shughuli zao, mtu Shilingi 5,000 na gari Shilingi 25,000, je, nini kauli ya Serikali kuhusu uhalali wa tozo hiyo?
Name
Eng. Ramo Matala Makani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI, MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dokta Shukuru Kawambwa Mbunge wa Bagamoyo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ushauri alioutoa nitaufikisha mbele ya Kamati hii maalum. Kwamba pamoja na utaratibu waliojiwekea wa kuweza kutimiza malengo yao kwa mujibu wa kazi walizopewa na hadidu za rejea.Ni jambo jema na ni wazo zuri na litaweza kuboresha matokeo ya kazi wanayoifanya kwa kuwashirikisha pia Mheshimiwa Mbunge pamoja ma Madiwani wanaohusika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili linlohusiana na TANAPA kuwatoza wananchi ada hizi; kwanza nalisikia kwa mara ya kwanza na kwa kuwa ni suala jipya kujua mantiki yake na sababu zake kwanini liko hivyo nahitaji muda kidogo, lakini kwa wakati huu nikiwa nimesimama hapa naliona lina ukakasi wa namna Fulani. Kwa hiyo namuomba Mheshimiwa Mbunge anipe nafasi, nalishughulikia mara moja katika kipindi hiki hiki cha Bunge na pengine kwasababu ya uzito wake kuwa mkubwa, mchana huu nikutane naye, nitakuwa nimeshafanya mawasiliano angalau ya awali kujua likoje halafu tuweze kutafuta suluhisho lake.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved