Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Khamis Mtumwa Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiwengwa

Primary Question

MHE. KHAMIS M. ALI aliuliza:- Kwa muda mrefu sasa baadhi ya wakuu wa Vituo vya polisi hasa Zanzibar hutumia pesa ao za mishahara kulipa huduma za umeme katika vituo hivyo; Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuwalipa au kuwarejeshea pesa wanazotumia kulipa umeme katika vituo hivyo?

Supplementary Question 1

MHE. KHAMIS M. ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza je. La kwanza, je Serikali haioni utaratibu huu wa askari au wakuu wa vituo kujaza fomu na kupeleka risiti unaonesha urasimu, na inapelekea hadi askari anastaafu kutokulipwa pesa zake hizi za kulipa umeme?
Lakini la pili kwa upande wa askari wadogo ambao si maafisa kwa nini wasiwekewe pesa zao za posho za umeme na maji katika mishahara yao kama wanavyofanya JWTZ? Nashukuru.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khamis Mtumwa, Mbunge wa Kiwengwa kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali lake la pili, ukweli ni kwamba sio askari wote ambao wanalipwa posho kuna askari ambao hawalipwi posho, kuna askari ambao wanaishi katika nyumba binafsi ambao ndio wengi. Kama unavyofahamu Waheshimiwa Wabunge sasa hivi tuna changamoto ya makazi kwa askari, ambao hawa kiutaratibu wanalipwa posho ya pango ni asilimia 15 ya mshahara. Kwa hiyo hawa hawana shida. Tatizo lilipo ni kwa wale askari ambao wanaishi kwenye nyumba za askari ambapo wakati mwingine kuna tatizo la kuchelewa kwa posho zao. Hata hivyo Serikali Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusiana na swali lake la kwanza ambapo alizungumzia kuchelewa kwa malipo hayo hadi kufikia wakati askari wanastaafu.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha ucheleweshwaji wa malipo ya madeni haya. Moja kama ambavyo mnafahamu wakati mwingine kunakuwa na ucheleweshaji wa kupata fedha za bajeti ama wakati mwingine zinakuja kidogo. Lakini pia wakati mwingine hata ambapo zinapokuja kuna matukio ambayo mara nyingi hatuyatarajii, ambayo yanajitokeza yanafanya matumizi yale yaweze kuhamishiwa na kutekeleza yale matumizi ya dharura, ikiwemo ya ujambazi, migogoro ya kijamii, hata operesheni za baadhi ya wanasiasa zisizokuwa na tija. Haya mambo na mambo mengine yanachangia wakati mwingine kufanya fedha hizi zitumike kwa matumizi mengine ya dharura na kuchelewesha malipo yale.