Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ruth Hiyob Mollel
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. RIZIKI S. MNGWALI (K.n.y MHE. MAGDALENA H. SAKAYA) aliuliza:- Wananchi wa Kitongoji cha Twende Pamoja, Kijiji cha Igwisi, Wilaya ya Kaliua wamekuwa wakipata athari kubwa za kiafya kutokana na milipuko ya baruti inayofanywa na Kampuni ya CHIKO, kupasua mawe na kokoto kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kaliua mpaka Kigoma:- (a) Kwa nini Serikali isiwalipe Wananchi hao stahiki zao ili waondoke sehemu hiyo na waende kuishi maeneo mengine ambayo ni salama? (b) Kijiji cha Igwisi kinanufaikaje na Machimbo haya ya Mawe ambayo yapo kwenye eneo hilo?
Supplementary Question 1
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru. Pamoja na majibu hayo, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. La kwanza, ni kwamba kwenye jibu lake la msingi la (b) anazungumzia malipo haya ya 2014, ni lini basi atatuambia pesa hizi zitalipwa ili Halmashauri ya Kaliua iweze kufanya shughuli zake kwa kutumia fedha hizo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni la ujumla, kwamba miradi kama hii inafanywa katika sehemu nyingi za nchi, lakini mara nyingi pamoja na kufanya social na environmental impact assessment bado wananchi huachwa mpaka wakapata mateso ndipo Serikali ikaja kuwalipa baadaye. Je, Serikali inatuambia nini kwamba sasa watakuwa wanafanya malipo kabla ya athari kupatikana kwa wananchi? Atupe majibu ni lini. Ahsante.
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa malipo ambayo yalitarajiwa kulipwa kwa kipindi hiki cha 2014 yangekuwa yameshafanyika hadi sasa, lakini hadi sasa hayajafanyika. Napenda nimpe uhakika Mheshimiwa Mbunge kwamba, TANROADS imeshafanya mahesabu na imeshamwandikia sasa mkandarasi kwa ajili ya kuanza malipo. Kwa sasa tumejipanga TANROADS pamoja na wenzetu, wataanza kulipwa kuanzia Agosti hadi Septemba mwaka huu kulingana na upatikanaji wa fedha
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali la pili kuhusiana na malipo kufanyika mapema. Kwa mujibu wa Sheria ya Madini ni kwamba kabla ya shughuli za madini hazijaanza kufanyika, kazi inayotakiwa kufanyika kwanza ni kufanya tathmini na tathmini ikishafanyika na malipo yakakubalika na wadau wakakubaliana kuhusiana na malipo ya fidia, kawaida malipo huwa yanafanyika kabla ya shughuli kuanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiri tu kwamba kwa sababu wakati wanaanza uchimbaji wa kokoto wa kwenye barabara hii, tathmini zilichelewa kukamilika, kwa hiyo, malipo hayakuanza kufanyika mapema. Hata hivyo, kwa taratibu ambazo tunaanza kuanzia sasa, malipo yatakuwa yanafanyika kabla ya wananchi kuathirika. Kwa hiyo, malipo ya fidia yatakuwa yakianza kufanyika kabla ya shughuli za uchimbaji wa kokoto kuanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi hatuwezi kusema zitaanza lini kwa sababu walishaanza kuathirika na malipo hayajafanyika, lakini malipo yote ambayo hayajafanyika kwenye barabara hii, yatafanyika kati ya Septemba hadi Oktoba mwishoni mwa mwaka huu bila kuchelewa kwa ushirikiano wa wadau, TANROADS pamoja na Halmashauri ya Kijiji.
Name
Savelina Slivanus Mwijage
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. RIZIKI S. MNGWALI (K.n.y MHE. MAGDALENA H. SAKAYA) aliuliza:- Wananchi wa Kitongoji cha Twende Pamoja, Kijiji cha Igwisi, Wilaya ya Kaliua wamekuwa wakipata athari kubwa za kiafya kutokana na milipuko ya baruti inayofanywa na Kampuni ya CHIKO, kupasua mawe na kokoto kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kaliua mpaka Kigoma:- (a) Kwa nini Serikali isiwalipe Wananchi hao stahiki zao ili waondoke sehemu hiyo na waende kuishi maeneo mengine ambayo ni salama? (b) Kijiji cha Igwisi kinanufaikaje na Machimbo haya ya Mawe ambayo yapo kwenye eneo hilo?
Supplementary Question 2
MHE. SAVELINA S. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru sana. Kwa kuwa milipuko hii inaleta matatizo ya afya ya wananchi walioko karibu na sehemu ya mashimo hayo na kuacha mazingira yakiwa na mashimo. Je, ni lini Serikali itakuwa inahakikisha afya za watu hao zinakuwa sawa?
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikubaliane nae kwanza, kwamba, shughuli za madini hufanyika na kuacha madhara kiafya. Kuhusu ni lini, ni wakati wote shughuli za madini zinapofanyika tunatakiwa tuhakikishe kwamba afya za wananchi pamoja na wachimbaji zinabaki salama.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved