Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kabula Enock Shitobela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, Serikali haina njia mbadala ya matumizi ya matimba kama ngazi ambayo yanamaliza miti na hivyo kuharibu mazingira?

Supplementary Question 1

MHE. KABULA E. SHITOBELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa kuna uwepo wa teknolojia mbadala, je, Serikali Serikali itaanza lini kutoa elimu ya matumizi ya matumizi ya teknolojia mbadala?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba matumizi ya teknolojia mbadala yapo na yanafanyika kwa wachimbaji wa kati na wakubwa lakini wapo pia wachimbaji wadogo ambao wana uwezo wa kununua mahitaji hayo, wanaendelea nayo. Sasa, sisi kama Wizara tunaendelea kutoa elimu ya uchimbaji salama kwenye migodi ikiwemo matumizi ya teknolojia mbadala.