Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zahor Mohamed Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwera
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza:- Je, lini Mifumo ya Malipo ya Kimataifa itaruhusiwa ili wabunifu/watu wanaofanya kazi za ushauri kwa taasisi za nje wapate malipo?
Supplementary Question 1
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya ziada. Namshukuru Waziri kwa jawabu lake zuri lakini ningeomba sasa Serikali ituambie, kwa sababu vijana wanapata tabu sana kupata malipo yao, Je, ni lini Serikali itaruhusu mifumo kama ya PayPal ili watu waanze kulipwa fedha zao? Ahsante. (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zahor kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Kampuni ya PayPal haijaomba leseni. Mara tu itakapoomba leseni na kukidhi vigezo vya kisheria basi Serikali itaruhusu kampuni hiyo kutoa huduma nchini.
Name
Issa Jumanne Mtemvu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibamba
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza:- Je, lini Mifumo ya Malipo ya Kimataifa itaruhusiwa ili wabunifu/watu wanaofanya kazi za ushauri kwa taasisi za nje wapate malipo?
Supplementary Question 2
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ilikuwa niseme kwa niaba yake kwa sababu aliwasiliana na mimi pia. Nakushukuru.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba hili tulichukue tukalifanyie kazi. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved