Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI K.n.y. MHE. ASYA SHARIF OMAR aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa huduma ya kifungua kinywa kwa wanafunzi wa shule za msingi?

Supplementary Question 1

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa vile tayari Serikali imeshatenga bajeti ya kutoa kifungua kinywa katika shule. Je, ni vipi Serikali itaangalia kwa uangalifu zaidi vifungua vinywa hivyo ambavyo vitatolewa katika shule hizo? Ahsante sana.

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza. Kwanza Serikali siyo kwamba imetenga bajeti kwa ajili ya vifungua kinywa, nilichokisema kwenye majibu yangu ya msingi ni kwamba Serikali kupitia Wizara ya Elimu, imetoa mwongozo wa namna gani ya kupata lishe ikiwemo wazazi wa maeneo husika kuchangia katika kupata lishe watoto hawa wakiwa shuleni.