Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prof. Shukrani Elisha Manya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Primary Question

MHE. PROF. SHUKRANI E. MANYA K.n.y. MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka vifaa kwenye Jengo Jipya la Mama na Mtoto katika Hospitali ya META Mkoani Mbeya?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. SHUKRANI E. MANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kukamilika na kuanza kutumika kwa jengo hilo kunaifanya Hospitali ya Kanda ya Mbeya kuongeza uwezo na ufanisi hata hivyo kuongeza pia viatanda kutoka 600 hadi 800.

Je, ni lini Serikali itakapoifanya Hospitali ya Kanda ya Mbeya kupata hadhi ya taasisi kama ilivyo MOI, JKCI na nyinginezo?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mchakato huo unaendelea wa kuifanya hospitali hiyo kuwa taasisi na bado tunaendelea mjadala, Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha na Utumishi kuona namna gani tunaweza kufikia hatua hiyo, ili nayo Mbeya iweze kuwa taasisi kama ambavyo hospitali nyingine za Kanda zinakuwa. (Makofi)