Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafanya tathmini ya kampuni zilizo chini ya NARCO ili kuona tija zake katika uchumi?
Supplementary Question 1
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali la nyongeza.
Kwa kuwa Serikali ina mpango wa kuendelea kuwapatia vijana wetu ajira; na kwa kuwa tumeona sehemu kubwa ya ranchi bado hazitumiki.
Je, Serikali haioni umuhimu wa kugawia vijana wetu maeneo ya kufuga na wakawafundisha ufugaji bora ili waweze kuwekeza sawa na wale wenzetu katika sekta ya kilimo walivyofanya? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mpango tulionao sasa hivi ni pamoja na kuongeza maeneo na kugawa maeneo ambayo hayatumiki kwa vijana ambao sisi Wizara ya Mifugo na Uvuvi tumepanga kufanya hivyo katika mwaka wa fedha unaokuja. Kwa hiyo, liko kwenye mpango na tunakwenda kulitekeleza, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved