Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya wafanyabiashara wa mazao ya misitu wanaozuiwa kufanya biashara na TFS?

Supplementary Question 1

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na nimpongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa majibu yao. Nitakuwa na swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa majibu yameonesha kanuni zipo na wananchi wanafahamu lakini kule bado kuna changamoto kwenye Jimbo la Kibaha Vijijini, je, Waziri atakuwa yuko tayari baada ya Bunge hili twende tukasaidiane kuwaelekeza kanuni na taratibu za uvunaji wa mazao hayo? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa wazo hili tunatamani sana tuendelee kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu umuhimu wa uhifadhi lakini kuwepo na uvunaji endelevu wa mazao wa misitu. Kwa hiyo natoa ukubali na utayari wa Wizara, tuko tayari kukutana na Wananchi wa Kibaha na maeneo mengine ili kutoa elimu na kuzungumza nao kwa ajili ya kutoa miongozo sahihi, ahsante.